Thursday 13 August 2015

UASIN GISHU

     Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Abdi Hassan amesema kuwa serikali inaendeleza shughuli ya kuwachunguza wanafunzi wote kutoka shule za msingi upili na vyuo vikuu kama njia moja ya kuimarisha usamala katika kaunti hiyo.

     Hassan amesema kuwa mwanafunzi yeyote yuleatakayeshukiwa kwa sababu ya mienendo yake atakamatwa ili kuwasaidia maafisa polisi katika uchunguzi na ripoti yoyote kuhusu uhalifu.

     Haya yanajiri baada ya vijana Zaidi ya ishirini kutoweka wengi wao wakiwa ni wanafunzi katika kaunti hiyo kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab majuma mawili yaliyopita.

     Hassan amewaomba wazazi wote ambao wanao wametoweka nyumbani kupiga ripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu nao

No comments:

Post a Comment